Duration 4:19

KIJANA MBUNIFU ATINGA POLISI CENTRAL DAR NA 'SUPRISE' AWASHANGAZA POLISI | Muungwana Tv

12 528 watched
0
59
Published 8 May 2020

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepokea msaada wa Mashine Maalum ya kutakasa mwili itakayotumiwa na askari na wageni wote wanaoingia katika kituo cha Polisi Kati Jiji DSM ili kuwakinga dhidi ya virusi vya Corona. Mashine hiyo inayoitwa kwa jina la kitaalam Corona Virus Disinfectant sanitizer spray imetengenezwa na kijana Mtanzania aitwae Gadios Mangana. Kijana huyo aliyetumia siku saba kuitengeneza Mashine hiyo na ameitengeneza kwa gharama ya shilingi laki nane tu za kitanzania na kuona ni bora atoe msaada kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwani anatambua kazi inayofanywa na Jeshi la Polisi, hivyo ni vema kuwakinga askari dhidi ya ugonjwa wa COVID 19 unaonezwa na virusi vya Corona. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam SACP-Lazaro Mambosasa akipokea Mashine hiyo kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro amemshukuru kijana huyo na kumpongeza kwa ubunifu wake.

Category

Show more

Comments - 19