...Chipsi Za Muhogo...
By Laylunnar Mo
...Mahitaji...
Muhogo fresh kiasi utakacho
Pilipili ya unga upendavo
Chumvi kiasi
Ndimu ya unga kidogo
Njugu za maganda upendavo
Mafuta ya kukaangia
...Mataarisho...
Menya maganda muhogo wako wote
Kisha ufute uzuri kwa tissue au kitambaa (usikoshe)
Chukua cha kuparia sehemu kubwa upare muhogo wako wote
Kisha tandaza uzuri kwenye sahani
Kama muhogo wako una maji na uko nchi za joto basi uanike kidgo tu usikauke kabisa
Au ukamue kidgo tu sio sana utavunjika
Kama hauna maji basi weka mafuta yako moto wa kiasi uanze kukaanga mpaka rangi upendayo uzitoe, kaanga zote umalize
Punguza moto ukaange njugu zako umalize
Wacha vote kwa tissue vitoke mafuta
Kwenye bakuli kubwa vunja vunja chips zako tartibu usivuruge, mimina njugu,chumvi, pilipili na ndimu ya unga kisha zipete uzuri na ukoroge na mwiko
Onja kuhakikisha zimekolea, kisha zihifadhi uzuri kwa bakuli la ufuniko au ziweke kwenye freezer bags.
Kula kwa mbatata, kwa chatne au chakua tu.
By Laylunnar Mo
By Laymoz's Zenji Delicacies
Kidokezo!
Ukitumia fryer hakikisha usiweke basket yako mpaka chini ukisha weka muhogo sababu mafuta yatapanda juu, zuia kwanza kwa juu yakisha pungua kasi utaiwacha chini, hii husababishwa na maji ya muhogo na starch yake.
🍲Enjoy
Category
Show more
Comments - 3
Related videos for Chips Za Muhogo/How to make cassava chips or chakri: